{"id":2601,"date":"2026-07-14T05:02:54","date_gmt":"2026-07-14T09:02:54","guid":{"rendered":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/?p=2601"},"modified":"2026-09-01T00:11:30","modified_gmt":"2026-09-01T04:11:30","slug":"sherehe-zinaonyesha-kuenea-kwa-kiswahili-kanada-lakini-maswali-yanabaki-kuhusu-ukuzaji-na-kuhifadhi-kiswahili-kwa-muda-mrefu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/2026\/07\/14\/sherehe-zinaonyesha-kuenea-kwa-kiswahili-kanada-lakini-maswali-yanabaki-kuhusu-ukuzaji-na-kuhifadhi-kiswahili-kwa-muda-mrefu\/","title":{"rendered":"Sherehe Zinaonyesha Kuenea kwa Kiswahili Kanada, Lakini Maswali Yanabaki Kuhusu Ukuzaji na Kuhifadhi Kiswahili kwa Muda Mrefu"},"content":{"rendered":"<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1030\" height=\"1030\" data-attachment-id=\"2608\" data-permalink=\"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/2026\/07\/14\/sherehe-zinaonyesha-kuenea-kwa-kiswahili-kanada-lakini-maswali-yanabaki-kuhusu-ukuzaji-na-kuhifadhi-kiswahili-kwa-muda-mrefu\/1000661630-2\/\" data-orig-file=\"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1.png\" data-orig-size=\"1254,1254\" data-comments-opened=\"0\" data-image-meta=\"{&quot;aperture&quot;:&quot;0&quot;,&quot;credit&quot;:&quot;&quot;,&quot;camera&quot;:&quot;&quot;,&quot;caption&quot;:&quot;&quot;,&quot;created_timestamp&quot;:&quot;0&quot;,&quot;copyright&quot;:&quot;&quot;,&quot;focal_length&quot;:&quot;0&quot;,&quot;iso&quot;:&quot;0&quot;,&quot;shutter_speed&quot;:&quot;0&quot;,&quot;title&quot;:&quot;&quot;,&quot;orientation&quot;:&quot;0&quot;,&quot;alt&quot;:&quot;&quot;}\" data-image-title=\"1000661630\" data-image-description=\"\" data-image-caption=\"\" data-large-file=\"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-1030x1030.png\" src=\"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-1030x1030.png\" alt=\"\" class=\"wp-image-2608\" srcset=\"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-1030x1030.png 1030w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-300x300.png?crop=1 300w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-100x100.png?crop=1 100w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-600x600.png?crop=1 600w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-330x330.png 330w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-360x360.png 360w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-768x768.png 768w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-1200x1200.png?crop=1 1200w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-800x800.png?crop=1 800w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-400x400.png?crop=1 400w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-200x200.png?crop=1 200w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-88x88.png 88w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-816x816.png 816w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1-80x80.png 80w, https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1.png 1254w\" sizes=\"auto, (max-width: 1030px) 100vw, 1030px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Na KHALID MAGRAM, Mwanzilishi na Mratibu wa Mwezi wa Urithi wa Kiswahili Ontario (Ontario Swahili Heritage Month)<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Sasa! baada ya tamasha lingine la Majira ya Kiangazi la Kiswahili (Swahili Summer Festival) kufikia tamati, vibanda vya mama lishe na wauzaji wa bidhaa mbalimbali za Afrika Mashariki kufunga virago vyao. Nini kitafuata? BBQ Picnic ya Simba dhidi ya Yanga!? Swali kwa wadau wa lugha ya Kiswahili je! nini baada ya hapo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baada ya maadhimisho ya pili ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inayotambuliwa na UNESCO, iliyoadhimishwa rasmi mwaka huu huko jijini Paris tarehe 7 Julai, na kufikia tamati yake mjini Toronto ambayo binafsi nilishuhudia jamii zinazozungumza Kiswahili zikikusanyika kuadhimisha siku hiyo kupitia matukio ya kitamaduni yaliyodhihirisha nafasi na umuhimu wa Kiswahili duniani.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Hapa Toronto, nilijiunga na mamia ya washiriki waliohudhuria Tamasha la kila mwaka la Swahili Summer Festival katika Kituo cha Pam McConnell Aquatic Centre. Tamasha hilo, lililoandaliwa na Swahili Cultural Centre, ulipata ujio wa wakilisha kutoka Baraza kuu la Kiswahili Tanzania (BAKITA). Lilijumuisha vyakula vya Afrika Mashariki, muziki, ngoma na maonesho ya mavazi ya kitamaduni, likiwavutia washiriki kutoka sehemu mbalimbali za diaspora.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Nilijionea mwenyewe uhai wa utamaduni wetu kupitia vivutio kama maonesho ya kanga, ngoma za asili na muziki wa Kiswahili, vilivyowapa wageni fursa ya kushuhudia utajiri wa urithi wetu.Kiswahili, kinachozungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 katika Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na sehemu za Kusini mwa Afrika, kinaendelea kupanua wigo wake duniani. Kwa mtazamo wangu, lugha hii\u2014iliyoundwa na karne nyingi za mwingiliano kati ya Pwani ya Uswahili\u2014pamoja na mchanganyiko wa lugha ya Kibantu, Kiarabu, Kiajemi na Kizungu. Kadhalika, ilienaendelea kupata nafasi muhimu katika elimu, diplomasia na biashara, huku ikiwa chombo madhubuti cha kujieleza kiutamaduni kupitia fasihi, muziki na simulizi za jadi.Hata hivyo, kupitia mazungumzo yangu na wanajamii pamoja na uchunguzi wangu wa maadhimisho haya, ninaona kuwa ingawa tamasha na sherehe hutoa mwonekano na kuhamasisha jamii, huenda zisitoshe kuhakikisha lugha inaendelea kuishi miongoni mwa vizazi vipya vya diaspora.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tusiridhike kwa sherehe za mara moja kwa mwaka. Tuingie mashuleni, vyuoni, tuanzishe stesheni\/vituo za redio na TV. Jamii yetu wapo wale wenye vipaji mbalimbali kwanini tusiwatafute na kuwapa fursa za kuitumikia jamii?<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Baada ya shughuli hizi za sherehe kumalizika, mara nyingi husikia wasiwasi kuhusu mwendelezo wa ushiriki wa jamii. Vijana wetu wengi wa kizazi cha pili na cha tatu hukabiliwa na changamoto ya kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha au kudumisha uhusiano imara na utambulisho wao wa kitamaduni. Bila fursa endelevu za kujifunza lugha na kushiriki katika programu za kitamaduni, ipo hatari ya Kiswahili kuhusishwa zaidi na sherehe za mara moja kwa mwaka badala ya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.Hali hii imeibua mjadala muhimu ndani ya jamii yetu kuhusu haja ya kuwa na mipango madhubuti na endelevu.Ninaamini<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ninaamini tunapaswa kuaanzisha madarasa ya Kiswahili, programu za vijana, fursa za ulezi (mentorship), pamoja na shughuli za kitamaduni kama usimulizi wa hadithi, sinema,maigizo na utayarishaji wa maudhui ya kidijitali. Kuanzisha mazingira ya mara kwa mara ya kutumia Kiswahili kutasaidia kuimarisha umuhimu wake kwa vizazi vijavyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kutokana na uzoefu wangu, kuhifadhi lugha hakutegemei maadhimisho ya kila mwaka pekee. Kunahitaji uwekezaji wa muda mrefu, ushirikiano madhubuti wa jamii na programu zinazofikika kwa wote ili kuhakikisha Kiswahili kinaendelea kustawi katika jamii za diaspora.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kadiri hamasa ya kujifunza na kutumia Kiswahili inavyozidi kuongezeka duniani, ninaona wito unaoongezeka kutoka kwa wanajamii wa kuwepo kwa juhudi za pamoja na zilizoratibiwa ili kuhakikisha mustakabali wa lugha hii unalindwa. Hii ni pamoja na kushirikiana na marafiki na viongozi wa serikali wanaotuunga mkono, kuanzisha vituo maalumu vya utamaduni na elimu ambapo Kiswahili kinaweza kufundishwa, kutumiwa na kuishi nayo kila siku, mwaka mzima.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na KHALID MAGRAM, Mwanzilishi na Mratibu wa Mwezi wa Urithi wa Kiswahili Ontario (Ontario Swahili Heritage Month) Sasa! baada ya tamasha lingine la Majira ya&#8230;<\/p>","protected":false},"author":137658691,"featured_media":2608,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":true,"template":"","format":"standard","meta":{"advanced_seo_description":"","jetpack_seo_html_title":"","jetpack_seo_noindex":false,"jetpack_seo_schema_type":"","_jetpack_newsletter_access":"","_jetpack_dont_email_post_to_subs":true,"_jetpack_newsletter_tier_id":0,"_jetpack_memberships_contains_paywalled_content":false,"_wpcom_ai_launchpad_first_post":false,"_jetpack_feature_clip_id":0,"_jetpack_memberships_contains_paid_content":false,"footnotes":"","jetpack_publicize_message":"","jetpack_publicize_feature_enabled":true,"jetpack_social_post_already_shared":true,"jetpack_social_options":{"image_generator_settings":{"template":"highway","default_image_id":0,"font":"","enabled":false},"version":2},"jetpack_post_was_ever_published":false},"categories":[785243811,785243905,785243820],"tags":[],"class_list":["post-2601","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-articles-from-swahili-speaking-community","category-culture","category-news-articles-in-kiswahili"],"jetpack_publicize_connections":[],"jetpack_sharing_enabled":true,"jetpack_likes_enabled":true,"jetpack_shortlink":"https:\/\/wp.me\/pfZiHJ-FX","jetpack_featured_media_url":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/wp-content\/uploads\/2026\/07\/1000661630-1.png","_links":{"self":[{"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2601","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/137658691"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2601"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2601\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2689,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2601\/revisions\/2689"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media\/2608"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2601"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2601"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/msimulizicommunitynews.ca\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2601"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}