Mwezi wa Ukombozi ni sehemu ya historia ya Afrika pia, Dewitt Lee awaambia Waafrika wa diaspora

Ashê | Mwanzilishi wa Caretakers of our Culture na mratibu wa ziara ya Bendera ya Ukombozi ya Amerika Kaskazini, Dewitt Lee, akisaini ombi la Mwezi wa Urithi wa Kiswahili katika hafla ya kupandisha bendera ya Ukombozi mjini Brampton, Ontario. Lee ni mfuasi mkubwa wa kuwafundisha kizazi kipya cha watu wenye asili ya Afrika lugha za mababu zao, ikiwemo Kiswahili. Picha imepigwa na Msimulizi

Msimulizi Community News imekuwa ikifuatilia kwa karibu maadhimisho ya Mwezi wa Ukombozi (Emancipation Month) — kuanzia sherehe za kupandisha bendera hadi mijadala ya kina kuhusu historia, haki na urithi wake. Na inabainika kuwa Agosti hubeba simulizi nyingi zaidi ya tunavyoweza kudhani. Msimulizi inawaletea taarifa zinazogusa nyanja zote za maadhimisho haya; kuanzia maana ya Mwezi wa Ukombozi kwa bara la Afrika lenyewe, hadi madai ya haki kwa watu wenye ulemavu yanayoibuliwa sambamba na Bendera ya Ukombozi.

Na tuanze kwa swali la msingi: Historia ya Ukombozi ni urithi wa nani?

Ukombozi na Urithi wa Afrika

Dewitt Lee, mwanzilishi wa mpango wa Ontario Emancipation Month and Flag Tour, anasisitiza kuwa historia ya Waafrika waliowekwa utumwani si historia ya diaspora pekee, bali ni urithi wa Waafrika wote duniani.

Akizungumza katika hafla ya kupandisha Bendera ya Ukombozi mjini Brampton, alisema:

“Tunapowatambua kama mababu zetu wenye mizizi Afrika, basi vizazi vyao vina mizizi hapa. Kama ambavyo Wakanada Weusi wanajivunia falme kubwa za Afrika kama Ghana, Mali na Misri, vivyo hivyo Waafrika wanapaswa kujivunia mababu wao waliovumilia, walipinga utumwa, walinusurika, na hatimaye wakaamua kubaki katika nyumba ya waliyowakandamiza.”

Kwa maneno hayo, Lee anatoa mwaliko wa wazi kwa jamii za Waafrika nchini Kanada kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Mwezi wa Ukombozi—si kama watazamaji, bali kama washiriki wenye nafasi na wajibu katika historia hiyo.

Kwa ufupi alisema:

“Hatuwezi kuipeperusha Bendera Nyeusi, Kijani na Nyekundu huku tukiiacha Afrika na Waafrika nje ya simulizi hilo.”

Stay Connected with Msimulizi

Get the latest news, stories and perspectives from the Swahili-speaking community in Canada, East Africa and the wider Swahili World.

We don’t spam! Read our privacy policy for more info.

Msimulizi is now on the Whattsup Channel. Click here

AI USE DISCLOSURE

Msimulizi Community News hutumia zana za akili bandia (AI) kusaidia katika utafiti, ukusanyaji wa taarifa, uundaji wa picha za infografia na vielelezo, pamoja na kuhariri na kuboresha baadhi ya makala. Waandishi wa habari na wahariri wetu wanaendelea kuwajibika kwa maudhui ya mwisho, uthibitishaji wa taarifa na maamuzi ya uhariri.

About the Author

KHALID MAGRAM
Diaspora media strategist, award winning journalist, community engagement, experience in strengthening connections between Canada and African communities.