USAJILI KWA AJILI YA MPANGO WA RUZUKU ZA JAMII KWA WAZEE WA ONTARIO 2027–2028

Older adults participating in games, crafts, exercise, and social activities

Wazee wa jamii mbali mbali kutoka diaspora za kiafrika wakiwa wanajishughulisha na michezo, sanaa na mazoezi ili kuondokana na kupunguza upweke katika moja ya vituo vya kijamii katika jimbo la Ontario.

KHALID MAGRAM, TORONTO, ON | Mashirika yasiyo ya faida (Non for Profit) na Taasisi za Diaspora sasa zinaweza kusajili kwa ajili ya Mpango wa Ruzuku za Jamii kwa Wazee wa Ontario (Seniors Community Grant Program) wa mwaka 2027–2028, ambao umetenga dola milioni 7 kusaidia wazee kuendelea kuwa na shughuli za kijamii, kuwa na afya bora na kudumisha uhusiano na jamii zao.

Mashirika yasiyo ya kifaida, serikali za manispaa, vyombo vya uongozi wa jamii za Wenyeji (Indigenous) pamoja na vikundi vya kijamii vinavyokidhi vigezo, vinaweza kuomba ruzuku ya hadi dola 25,000 kwa ajili ya kuendesha programu na shughuli zinazolenga wazee wenye umri wa miaka 55 na zaidi.

Fedha hizo zinaweza kutumika kusaidia mipango mbalimbali, ikiwemo shughuli za kijamii na burudani, mafunzo ya matumizi ya teknolojia na ujuzi wa kidijitali, programu za afya na ustawi, elimu ya kujikinga dhidi ya utapeli, fursa za kujitolea pamoja na shughuli zinazowaleta pamoja wazee na vizazi vijana.

Katika mwaka huu, programu hiyo pia imetenga dola milioni 1 maalumu kwa ajili ya kuboresha maisha ya maveterani wazee.

Mashirika ya kijamii ya diaspora yanahimizwa kushirikiana, kuwasilisha maombi na kuibua miradi inayolenga kusaidia wazee wa maeneo yao ili kupunguza upweke na kutengwa kwa jamii.

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi: Desemba 17, 2026.

Jifunze zaidi na uwasilishe ombi hapa

Kama unataka kupata habari za jamii ya Waswahili na diaspora ya Afrika Mashariki wanaoiishi Kanada, jisajili ili tukutumie jarida (Newsletter) letu la kila wiki moja kwa moja kwenye inbox yako. Pia unaweza acha ujumbe kwenye comment kuhusu stori gani unataka Msimulizi azifuatilie! Tutahakikisha kuzichapisha hapa.

Usisahau kumpelekea mshikaji wako habari hii, Asante.

Endelea Kuwa Unganishwa na Msimulizi

Discover the stories connecting Canada, East Africa and the wider Swahili world.

Get community news, diaspora voices, cultural stories and perspectives on business, heritage and opportunities across borders — delivered straight to your inbox.

We don’t spam! Read our privacy policy for more info.

Msimulizi is now on the Whattsup Channel. Click here

AI USE DISCLOSURE

Msimulizi Community News hutumia zana za akili bandia (AI) kusaidia katika utafiti, ukusanyaji wa taarifa, uundaji wa picha za infografia na vielelezo, pamoja na kuhariri na kuboresha baadhi ya makala. Waandishi wa habari na wahariri wetu wanaendelea kuwajibika kwa maudhui ya mwisho, uthibitishaji wa taarifa na maamuzi ya uhariri.

About the Author

KHALID MAGRAM
Diaspora media strategist, award winning journalist, community engagement, experience in strengthening connections between Canada and African communities.

Be the first to comment on "USAJILI KWA AJILI YA MPANGO WA RUZUKU ZA JAMII KWA WAZEE WA ONTARIO 2027–2028"

Leave a comment