Magonjwa zaidi ya 150 Yameiidhinishwa na Serikali ya Kanada ili kuwapatia Walioathirika Mstakabali Mwema
Jumuiya za Wahamiaji nyingi nchini Kanada zinakosa zana muhimu ya kifedha iliyoundwa kusaidia watu wenye ulemavu.
Mpango Uliosajiliwa wa Akiba ya Walemavu (Registered Disability Savings Plan-RDSP). Mpango huu wakuwasaidia watu walio na ulemavu unapatikana tangu 2008, lakini wataalam wanasema bado hautumiki kwa kiasi kikubwa, hasa miongoni mwa jamii mbalimbal za Wahamiaji hapa nchini.
Kwa mujibu wa Takwimu za Kanada, ni asilimia 32 pekee ya Wakanada wanaostahiki (hadi umri wa miaka 59) walikuwa na RDSP mwaka wa 2020. Kikwazo kimoja kikuu ni ukosefu wa ufahamu.
Kizuizi cha lugha kina mchango mkubwa katika ukosefu wa ufahamu kuhusu RDSPs miongoni mwa jamii za Wahamiaji.
Wageni wengi wanaokuja Kanada wanaweza wasijue Kiingereza au Kifaransa vizuri, na hivyo kufanya iwe vigumu kwao kupata taarifa kuhusu programu na huduma za serikali, ikiwa ni pamoja na RDSP.
“Nimekuwa najishughulisha kwa muda mrefu sasa kuwapatia zana hii muhimu kwa watu waliokuwa na ulemavu na wale wanaostahiki,” anasema Alex Marifoglou, Meneja wa Tawi la Primerica Life Insuarance Company of Canada mjini, London, ON.
“Tungependa sana kukutana na viongozi na wana jamii za Wahamiaji ili tuwaandalie workshop kuwaelimisha kuhusu RDSP,” anasema Alex.
Zaidi ya hayo, tofauti za kitamaduni na viwango tofauti vya ujuzi wa kifedha vinaweza pia kuchangia pengo la maarifa. Kwa hiyo, watu binafsi na familia nyingi kutoka asili tofauti wanakosa fursa hii muhimu ya kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
RDSP inatoa ruzuku kwa ukarimu na dhamana za serikali ili kuwasaidia watu wenye ulemavu kujizatiti na maisha yao ya baadaye. Taasisi kuu za kifedha za Kanada zote hutoa RDSP, na serikali ya shirikisho hutoa aina mbili za motisha: Ruzuku ya Akiba ya Walemavu ya Kanada (CDSG) na Dhamana ya Akiba ya Walemavu ya Kanada (CDSB).


Advertising
Msimulizi is now on the Whattsup Channel. Click here
Msimulizi Community News uses artificial intelligence (AI) tools to assist with research, information gathering, infographic and illustrative images, and editing/polishing of some articles. Our journalists and editors remain responsible for the final content, verification and editorial decisions.
Discover more from Msimulizi Community News
Subscribe to get the latest posts sent to your email.
You must be logged in to post a comment.