AI Kutuangamiza Sote! Onyo kutoka Wataalamu.

Sisi kama jamii tumejitayarisha vipi kukabiliana na mapinduzi ya Akili Bandia?

Hivi karibuni wadau na wataalamu mbalimbali wamejitokeza kudai kuwa binadamu anacheza pata potea na teknolojia ya Akili Bandia (AI) na wametoa onyo kama teknolojia hiyo haijadhibitiwa inaweza kuleta maafa makubwa duniani.

Katika miongo iliyopita kuna mapinduzi mbalimbali ikiwemo mapinduzi ya viwanda yalioleta mabadiliko makubwa kwenye maisha ya binadamu.

Mapinduzi ya Viwanda yalibadilisha kabisa muelekeo wa jamii zilizokuwa zikitegemea kilimo. Athari zingine za mapinduzi hayo mpaka leo hii yanajaribiwa kuusuluhishwa bila ya mafanikio. Kama vile mabadiliko ya tabianchi ni moja ya athari nyingi za Mapinduzi ya Viwanda.

Kama ilivyo tokea hapo awali Mapinduzi ya Akili Bandia pia italeta mabadiliko makubwa duniani. Fununu zipo nyingi tu!. na tumeaaza kuziona katika maisha yetu ya kila siku.

Pamoja mimi na wewe tumejitayarisha vipi kukabiliana nayo?

Hapa nimeona meseji ya nukuu hiyo hapo chini ya George Santayana itanisaidia katika kutia maanani maada ya leo.

“Those who cannot remember the past are condemned to repeat it.” — George Santayana

“Wale wanaosahau yaliyopita wako katika hatari ya kurudia makosa yale yale.” – George Santayana

Kama wewe ni mtaalamu wa mambo ya teknolojia na unalo la kusema kuhusu Akili Bandia (AI) panda jukwaani ili viongozi wa jamii wakusikie! Viongozi wetu wa jamii nao wanajukumu la kutafuta njia za kuelimisha jamii kwa kutayarisha warsha na kongamano za wataalamu mbalimbali wa teknolojia pale inapowezekana ili kuelimisha jamii kuepukana na athari za Akili Bandia.

Ukiamini au usiamini onyo la wataalamu, ukweli ni kwamba muongo ujao utakuwa na mwelekeo tofauti sana kulinganisha na muongo huu. Jamii zitakazowahi kuchukua hatua watakuwa katika nafasi nzuri za kupunguza athari zisizoepukana.

Msimulizi is now on the Whattsup Channel. Click here

AI USE DISCLOSURE

Msimulizi Community News uses artificial intelligence (AI) tools to assist with research, information gathering, infographic and illustrative images, and editing/polishing of some articles. Our journalists and editors remain responsible for the final content, verification and editorial decisions.


Discover more from Msimulizi Community News

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

About the Author

KHALID MAGRAM
Diaspora media strategist, award winning journalist, community engagement, experience in strengthening connections between Canada and African communities.

Be the first to comment on "AI Kutuangamiza Sote! Onyo kutoka Wataalamu."

Leave a Reply